Kiswahili Insha Examples

Looking for Kiswahili Insha Examples? Want to set exams for your class and have no idea on Isha to set.

Below are some Kiswahili Insha Examples that you can use.

Kiswahili Insha Examples

Insha Za Darasa La Nane

1.

Umepewa dakika 40 Kuandika Insha yako.

Endeleza isha ifuatayo kwa naneo yasiyopungua ukurasa mmona na nusu

Alfajiri hiyo tulidamka tukiwa na furaha kama tasa aliyepata mwana. Tulikuwa tukisafiri kwenda ……………………………………………………………

 

2.

Maagizo: Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukifuata maagizo uliyopewa

Umechaguluwa kutoa hotuba kwa niaba ya wanafunzi wenzako siku ya kuombea watainiwa shuleni mwenu. Andika hotuba yako …………………………………………………………………………………………………………………………………………

 

3.

Umepewa dakika 40 Kuandika Insha yako.

Andika inhs isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukifuata maagizo uliyopewa.

Anza isha yako kwa

Kwa kweli niligundua kuwa mungu alikufunga nafasi hapa, hufungua kwingine …………………………………………………………………………………………………………………………………………

Read: Methali za Kiswahili

4.

Umepewa dakika 40 Kuandika Insha yako.

Andika inhs isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukifuata maagizo uliyopewa.

Mwandikie rafiki yako barua ukimshauri kuhusu namna ya kujiandaa vyema kwa mtihani wa KCPE

…………………………………………………………………………………………………………………………………………

See also: KCPE Insha revision

Kiswahili Insha Examples Insha Za Methali

 • Wema Hauozi
 • Kwendako mema hurudi mema
 • Akili ni mali

Insha ya Methali

Akili ni Mali

Methali hii chambilecho wahenga na wahenguzi ina maana kuwa mtu akitumia akili zake vyema mwishowe anafanikiwa maishani.

Hapo zamani za kale palikuwa na kijiji kimoja kilichokuwa kichafu mno. Kijiji hicho kilijulikana kama Mapengoni. Kilikuwa na panya wengi waliokuwa wanaishi na babu yao. Panya hao walikuwa wengi kiasi cha kutohesabika. Kila mchana walisherehekea kula vyakula tofauti, na kwa vile walikuwa wengi walikuwa wakila vyakula vingi. Kwa tabia yao ya kula kila wakati, panya hao walinona kama nguruwe.

Karibu na kijiji cha Mapengoni paliishi paka mmoja mnene sana. Paka huyo alikuwa mweusi tititi lakini macho yake yalikuwa meupe kama theluji. Mara kwa mara paka huyo alikuwa akiwakamata panya wachache na kuwala. Siku zilipita na paka aliendelea kuwala panya bila kusita.

Siku moja panya walifanya mkutano ilikujadili namna ya kumzuia paka kuwala kila mara. Panya mmoja mdogo alisamama na kusema“ndugu zangu tunaweza tengeneza kengele ambayo tutamfunga paka shingoni ilituwe tukimskia kila anapo wasili.” Panya wengine walisikiza kwa makini na walifurahia wazo la mwenzao. “nani atamfunga paka kengele?“ Panya mmoja mkongwe aliuliza. Kwa kweli panya wengine walistaajabu kwa vile hawakujua jinsi ya kuifunga kengele kwa shingo ya paka.

Baada ya majadilaino, panya aliyetoa wazo la kengele alisamama na kujitolea kumfunga paka kengele. Panya wengine walimshangilia huyo panya mdogo. Alipoenda nyumbani panya huyo aliwaza na kuwazua jinsi ya kuifanya kazi aliyo ahindi wenzio. Mawazo yalimjaa na siku moja wazo kuu lilimjia akilini. Aliona shimo moja karibu na lango kuu la kuingia kijijini. Shimo hilo lilikuwa linaupana wa kutoshea kichwa cha paka.

Ili kutimiza wazo lake, panya huyo aliwakusanya wenzake na kuwashauri wajifungie kwenye nyumba zao kwa muda wa wiki mbili. Aliwaliifu wakusanye vyakula vya kutosha. Baada ya kukusanya vyakula vya kutosha, panya walijifungia. Kila paka alipopita karibu na kijiji cha mapengo aliskia kila kitu kimetulia tuli. Wiki ya kwanza ilipo kwisha paka alifika kwenye lango kuu na kutupa macho ilikuona kama kuna jambo lilikuwa likiendelelea. Yule panya mdogo alijificha nyuma ya lango kuu, akisubiri ile siku paka atajaribu kuingiza kichwa chake kwenye lile shimo. Njaa ilipozidi, paka alirudi na kusubiri kwenye lango, lakini hakuna panya aliyotoka.

Hatimaye paka aliingisha kichwa chake kwenya lile shimo, mara moja panya alimfunga kengele. Kufumba na kufumbua paka alijipata na kengele shingoni. Alijaribu kutikisa kichwa ilikuitoa ile kengele lakini hakufaulu. Kengele ililia kwa kelele sana na yule panya mdogo alingashilia kwa shangwe na nderemo. Aliwaita wenzake wote na walimuona paka akitoroka huku akiwa na kengele. Kwa kweli baada ya dhiki faraja, panya hao walisherekea sana. Kutoka siku hiyo panya waliweza kujificha kila mara walipoisikia kelele za kengele. Wahenga walinena waliposema akili ni mali.

Read: KCPE Kiswahili Revision Paper With Answers

Kiswahili Insha Examples Insha za Mjadala

Insha ya mjadala humhitaji mwanafunzi atoe maoni yake kuunga mada na pia kupinga kauli fulani. Katika insha za aina hii, mwanafunzi anaweza kuegemea upande mmoja tu ikiwa upande wa kupinga hauna hoja za kutosha.

Insha za Kubuni

Insha za ubunifu ni insha ambazo mwanafunzi huhitaji kubuni maudhui, mazingira, wahusika, na kadhalika kulingana na swali analorejelea. Insha hizi zinaweza kuwa za methali, mdokezo ama insha zenye mada ambazo hazina mtindo rasmi.

Insha za Mdokezo

Hizi ni Insha za ubunifu ambazo mwanafunzi hupewa kifungu cha maneno kinachopaswa kujitokeza katika insha yake.

Baadhi ya insha za aina hii huwa zimetangulizwa na mwanafunzi hutakiwa akamilishe na nyinginezo huwa na kimalizio. Japo mwanafunzi ana uhuru wa kuiendeleza insha yake atakavyo, ni sharti ajifunge katika maudhui yanayojitokeza katika mdokezo aliopewa. Kwa hivyo, kabla ya mwanafunzi kuiendeleza insha yake, ni sharti atambue maudhui yaliyokusudiwa na mtahini.

Kwa mfano:

Endeleza insha ifuatayo na uifanye iwe ya kuvutia:

 1. Nikasikia sauti hiyo tena. Sikuamini masikio yangu. Moyo ukaanza kunienda mbio mbio. Mara upepo….
 2. Giza lilikuwa limechukua milki ya viumbe wote duniani. Nyota zilitoa mwanga hafifu na mwezi ulikuwa ushatua. Katika giza hilo la kaniki….

Find: Free 2021 KCPE Math Past Papers with Answers

Insha za Mada

Hizi ni insha ambazo mwaandishi hutakiwa kuzungumzia mada fulani kwa kutoa hoja ama maelezo. Insha hizi hazimhitaji mtahiniwa kuanza kusimulia hadithi yake bali ni kurejelea mada aliyopewa. Mwandishi wa insha kama hii anapaswa kuwa na hoja za kutosha kuhusu mada aliyopewa kabla ya kuanza kuiandika. Hoja zote zinapaswa kujitokeza katika masimulizi yenye mtiririko wala si kuorodhesha hoja, moja baada ya jingine.

Kwa mfano:

Andika insha juu ya:

 1. Umuhimu wa kupanda miti
 2. Athari za kuavya mimba
 3. Namna ya kuboresha kilimo katika sehemu zenye ukame
 4. Mbinu za kukabiliana na wezi wa mifugo.

Insha hizi huwa insha halisia na hivyo mwaandishi hawezi kupigia chuku au kutoa hoja zisizo kweli. Kwa mara nyingi insha hizi hurejelea maswala ibuka katika jamii k.v njaa, ukimwi, kilimo, ufisadi, ukabila, n.k

Hata hivyo mwanafunzi anaweza kupata insha za mada zinazohitaji ubunifu, mapambo ya lugha n.k. Angalia mifano ifuatayo.

Andika insha juu ya:

 1. “Ndoto Niliyokuwa Nayo”
 2. “Siku Ambayo Sitaisahau Maishani”
 3. “Sherehe Niliyoihudhuria”
 4. “Ajali ya Barabarani Niliyoishuhudia”

Download: Free 2021 KCPE English Past Papers with Answers

Insha Ya Mada Teule

 • Eleza maafa ya ukimwi nchini mwako.
 • Faida za michezo
 • Faida za muziki
 • Faida na madhara ya utalii nchini
 • Kiini cha ajali barabarani nchini
 • Kazi niipendayo

Insha za Mahojiano

Hizi ni insha ambazo mhusika mmoja huwa akimhoji au kumwuliza maswali mwenzake.

 1. Mahojiano ya mtu anayeomba kazi
 2. Mahojiano baina ya askari na shahidi kuhusu kisa cha mauaji
 3. Mahojiano baina ya mwaandishi wa habari na mwananchi kuhusu katiba mpya
 4. Mahojiano baina ya daktari na mgonjwa

How to pass KCSE Insha paper

Kila mwaka wanafunzi wa kidato cha nne pamoja na wale wa darasa la nane huandika insha kama jinsi ya kutahiniwa uwezo wao wa kuwasiliana. Ili kupita na kupata alama za juu, wnafunzi wanaffa kuwasilisha ujumbe sahii wakiyumia lugha ya kuvuitia na yenye mawazo asili.

KCSE Insha questions

Maswali ya insha huwa ni manne

 1. Swali la kwanza huma nila lazima na huwa linahusu insha kiuamilifu

Example of insha kiuamilifu questions

Mfano wa maswali ya insha kiuamilifu

 • Barua za Kirafiki
 • Barua rasmi
 • Barua pepe
 • Wasifu
 • Tawasifu
 • Tawasifu kazi
 • Ilani
 • Tahariri
 • Mahojino
 • Mazungumzo
 • Kumbukumbu
 • Ratiba
 • Hotuba
 • Ripoti rasmi
 • Risala

Find: Free 2021 KCPE Kiswahili Past Papers with Answers

 1. Swali la pili huhusu masuala inuka katika jamii na huhusisha mjadala, maelezo ya kina na ufafanuzi

Mfano wa maswali katika sehemu ya pili ya insha

Ufisadi, Ukosefu wa ajira, ugatuzi, utumizi wa simu, Kilimo dhabiti

 1. Swali la tatu huhusu methali
 2. Swali la nne huwa insha ya kubuni ama mmdokezo

Tips on how to pass Kiswahili Insha paper

Kila swali la insha huhitaji kichwa ambacho hudokeza mada inayofafanuliwa katika mwili wa insha. Watahiniwa wengi hufanya makosa wanapoandika kichwa. Hili huwakosesha alama au kuwapungunguzia alama

 • Mtahiniwa asiweke kitone au nukta baada ya kichwa cha insha
 • Kichwa kisipite mamaeno sita katika swali la pili, tatu na nne
 • Katika insha kiuamilifu kichwa kinawaeza kuzidi maneneo sita
 • Katika insha kiuamilifu aghalabu kichwa kianze kwa kutaja aina ya insha
 • Katika swali la tatu mtahiniwa atumie methali aliyopewa kama kichwa. Asitumies methali mbadala
 • Katika swali la tatu mtahiniwa atoe kihwa kulinagana na mameno ya mdokezo
 • Mtahiniwa aandike kichwa kwa herufi kubwa na akipige mstari

Find: Free 2021 KCPE Social Studies Past Papers with Answers

Insha za Kiswahili

1997-2017 KCSE compulsory insha past papers

 

 1. 1997 KCSE Insha past papers

Ripoti

Ulikuw akiongozi wa timu yako katika mashindano ya riadha katika mkoa. Andika ripoti kwa mwalimu mkuu kuhusu mamabo wyalivyokuwa

 1. 1998 KCSE Insha past papers

Masuala ibuka

Eleza madhara yatokanayo na vijana kujiingiza katika ulevi wa aina mbalimbali na upendekeze hatua zifaazo kuchukuliwa ili kuliondoa tatizo hili

 1. 2000 KCSE Insha past papers

Mazungumzo

Andika mazungumzo kati ya mwalimu mkuu, mwanafunzi na mzazi wake kuhusu kuzorota kwa kazi na tabia ya mwanafunzi huyu shuleni

 1. 2001 KCSE Insha past papers

Hotuba

Umekaribishwa kuwa mgeni wa heshima katika kata yenu. Andika hotuba kuhusu matatizo yanayowakumba watoto wa shule na kusababisha wengine kuacha shule hatimaye kufanya kazi zilizizidi umri wao

 1. 2002 KCSE Insha past papers

Masuala ibuka

Jukumu la kuwafundisha vijana maadili ni la mzazi na pia watu wengine katika jamii. Fafanua

 1. 2003 KCSE Insha past papers

Mazungumzo

Umekutana na rafiki yako miaka miwili baada ya kumaliza kidato cha nne. Mna mengi ya kuzungumza kuhusu vile mnavyoendelea maishani. Andika mazungumzo yenu

Kiswahili insha Examples KCSE

 1. 2004 KCSE Insha past papers

Kumbukumbu

Baada ya matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwalimu mkuu alwaita wazazi na wanfunzi shuleni kuyajadili matokeo hayo. Andika kumbukumbu za mkutano huo

 1. 2005 KCSE Insha past papers

Hotuba

Andika hotuba kuhus matatizo ya maji kijijini au kitongojini mwenu na suluhisho lake utakayotoa katika sherehe ya kuandimisha siku ya maji duniani

 1. 2006 KCSE Insha past papers

Ripoti rasmi

Umealikwa kuwa katibu wa kamtai inayotoa mapendekezo ya jinsi ya kupambana na tatizo sugu la dawa za kulevya. Andika ripiti yako

 1. 2007 KCSE Insha past papers

Barua kwa mhariri

Andika barua kwa mhariri wa gazeti ukilalamikia hali ya watu nchini kwenu ili kumwendeleza kielimu mtoto msichana

 1. 2008 KCSE Insha past papers

Tahariri

Andika tahariri kwa gazeti la Raia ukieleza hatua zinazochukuliwa nchini ili kumwendeleza kielimu mtoto msichana

 1. 2009 KCSE Insha past papers

Hotuba

Umealikwa kitongoni mwenu kama mgeni wa heshima katika hafla za kuzindua kundi la wasanii wa kikwetu. Andika hotuba utakayotoa ya kuonyesha umuhimu wa sanaa na michezo

 1. 2010 KCSE Insha past papers

Wasifu

Andika wasifu wa ndugu yako ambaye amepanga hafla ya kuchangisha pesa za kumgharamia masomo ya Chuo kukuu

 1. 2011 KCSE Insha past papers

Mahojiano

Wewe kama mwanafunzi umeota nafasi ya kumhoji Mkurugenzi wa habari nchini kuhusu umuhimu wa magazeti kwa wanafunzi wa shule za sekondari. Andika mahojiano hayo

 1. 2012 KCSE Insha past papers

Kumbukumbu

Wewe ni mkuu wa Baraza la Wanafunzi shuleni mwenu. Kumekuwa na visa vya wanafunzi kukiuka sharia za shule. Andika kumbukumbu za mkutano wa baraza hili uliofanya kujadili suala hili

 1. 2013 KCSE Insha past papers

Memo

Wewe ni meneja wa kampuni ya jitihada ambapo pamekubwa na visa vya ukiukaji na maadili ya kikazi. Waandikie wafanyakazi memo kuwaonya dhidi ya jambo hili

 1. 2014 KCSE Insha past papers

Hotuba

Andika hotuba utakayowatolea wazazi, walimu na wanafunzi kuhusus umuhimu wa ushauri-nasaha katika shule za sekondari

 

 1. 2015 KCSE Insha past papers

Ripoti

Andika ripoti kuhusus vyanzo vya wanafunzi kuacha shule kabla ya kukamilisha masomo yao katika eneo la Tekeleza

 1. 2016 KCSE Insha past papers

Ripoti

Kumekuwa na visa vya matumizi ya dawa za kulenya. Andika ripoti huku ukipendekeza namna ya kuzuia madhara hayo

 1. 2017 KCSE Insha past papers

Barua kwa mhariri

Kuna kiwanda cha kutungeneza matofali katika jimbo lako. Mwandikie mhariri wa gazeti la Nyota ukimwelezea changamoto na faida ya kiwanda hicho

Insha Za Darasa La Nne

 1. Rafiki Yanyu
 2. Siku Ambayo Sitasahau
 3. Mnyama nimpendaye
 4. Umuhimu wa miti
 5. Familia Yangu