Methali za Kiswahili

Searching for Methali za Kiswahili. Today we are going to look at Methali za Kiswahili. You can use them in your saying or writing Isha.

A

 • Ada ya mja hunena, mwungwana ni kitendo.
 • Adhabu ya kaburi aijua maiti
 • Afua ni mbili, kufa na kupona.
 • Ahadi ni deni.
 • Aibu ya maiti, aijua mwosha.
 • Ajali haina kinga wala kufara
 • Aisifuye mvua, imemnyeshea.
 • Akiba haiozi.
 • Ajidhaniye amesimama, aangalie asianguke.
 • Asifuye mvuwa imemnyea.
 • Akili nyingi huondowa maarifa.
 • Akili ni nywele; kila mtu ana zake.
 • Akitaka kaa, mpe moto.

Read: Kiswahili Insha Examples

 • Akipenda chongo huita, huona kengeza.
 • Akufukuzaye hakwambii, Toka.
 • Akupaye kisogo si mwenzio.
 • Akumulikaye mchana; usiku akuchoma.
 • Aliyekando, haangukiwi na mti.
 • Alalaye usimwamshe; ukimwamsha, utalala wewe.
 • Aliyeko juu, mungojee chini.
 • Amani haipatikani ila kwa ncha ya upanga.
 • Amnyimae punda adesi, kampunguzia mashuzi.
 • Asiye kuwapo na lake halipo.
 • Asiyefunzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu
 • Asiyekuwapo na lake halipo.
 • Asiyekujua hakuthamini.
 • Asiye kubali kushindwa si mshindani.
 • Asiyesikia la mkuu, huvunja guu
 • Atangaye na jua hujuwa.
 • Avumaye baharini papa kumbe wengi wapo.
 • Avuaye nguo huchutama.

B

 • Baada ya kisa mkasa. Baada ya chanzo kitendo.
 • Baniani mbaya kiatu chake dawa.
 • Baada ya dhiki faraja.
 • Bendera hufuata upepo.
 • Baniani mbaya kiatu chake dawa.
 • Bora afya kuliko mali.
 • Bilisi wa mtu ni mtu.

Read: KCPE Kiswahili Revision Paper With Answers

C

 • Chanda chema huvikwa pete.
 • Chamlevi huliwa na mgema.
 • Cha kuvunda, hakina ubani.
 • Chema chajiuza, kibaya chajitembeza
 • Chombo cha kuzama hakina usukani.
 • Chembe na chembe ni mkate.
 • Cha kichwa kitamu, na cha mkia kitamu.
 • Chovya chovya yamaliza buyu la asali.
 • Cha kuvunja, hakina rubani.
 • Chema hakikai
 • Chombo kilichopikiwa samaki hakiachi kunuka vumba.
 • Chui hageuki madoamadoa
 • Chungu kikuu, hakikosi ukoko.

Read: African Proverbs

D

 • Dalili ya mvua mawingu.
 • Dau la mnyonge haliendi joshi; likienda joshi ni mungu kupenda.
 • Damu nzito kuliko maji.
 • Debe shinda haliachi kutika.
 • Dawa ya moto ni moto.
 • Dunia duwara.
 • Dua la kuku halimpati mwewe.
 • Duniani ni msiba na furaha, kuna ugonjwa na siha.
 • Dunia huleta jema na ovu.
 • E
 • Elimu bahari, haina kuta wala dari.
 • F
 • Fadhila ya punda ni mateke.
 • Faragha ya nyani, huishia ngokoni
 • Fimbo ya mbali hayiuwi nyoka.
 • Fahali wawili hawakai zizi moja.
 • Fuata nyuki ule asali.
 • Fedha fedheha.
 • Fumbo mfumbe mjinga mwerevu huligangua.
 • Fungato haliumizi kuni.

Read: Debate Motions for Secondary Schools in Kenya

G

 • Ganda la mua la jana chungu kaona kivuno.

H

 • Haba na haba hujaza kibaba.
 • Habari ya uwongo, ncha zake saba, habari ya kweli, ncha yake moja.
 • Hapana marefu yasio na mwisho.
 • Hakuna bahari, isiyo na mawimbi.
 • Hakuna siri ya watu wawili.
 • Haraka haraka haina baraka.
 • Hasira, hasara.
 • Hasira za mkizi, tijara ya mvuvi
 • Hakuna kisicho badali.
 • Heri kufa macho kuliko kufa moyo.
 • Heri kujikwa kidole kuliko ulimi.
 • Hiari ya shinda utumwa.
 • Hucheka kovu asiye kuwa na jeraha.
 • Hapana marefu yasio na mwisho.
 • Heri kuliwa na simba, kuliko kuliwa na fisi.
 • Hucheka kovu asiye kuwa na jeraha.

J

 • Jina jema hungara gizani.
 • Jitihadi haiondoi kudura ya mungu.
 • Jogoo la shamba haliwiki mjini.
 • Jino la pembe si dawa ya pengo.
 • Jivu halijai, gao la mkono.

Read: CBC Curriculum Structure

K

 • Kamba hukatika pabovu.
 • Kafiri akufaye si Isilamu asiyekufa.
 • Kama chanda na pete.
 • Kanga hazai ugenini.
 • Kata pua uunge wajihi
 • Kawia ufike
 • Kazi mbaya siyo mchezo mwema.
 • Kelele za mlango haziniwasi usingizi.
 • Kenda karibu na kumi.
 • Kidole kimoja hakivunji chawa.
 • Kidogo ni tamu, kingi ni sumu.
 • Kichache hakikutoshi na kingi hakikulishi.
 • Kiburi si maungwana.
 • Kikulacho ki nguoni mwako.
 • Kila mlango na ufunguo wake.
 • Kila chombo kwa wimbile.
 • Kingiacho mjini si haramu.
 • Kila ndege huruka na mbawa zake.
 • Kimya kingi kina mshindo mkubwa.
 • Kinyozi hajinyoi, akinyoa kujikata.
 • Kipendacho moyo ni dawa.
 • Kipofu haonyi njia.
 • Kila mwamba ngoma ,ngozi huivuta kwake.
 • Kila ndege mwenye mkia ni lazima aringe.
 • Kilio huanza mfiwa ndipo wa mbali wakaingia.
 • Kinga na kinga ndipo moto uwakapo.
 • Kinolewacho, hukata.
 • Kilichomo baharini, kakingojee ufukoni.
 • Kiozacho hutoa uvundo
 • Kipofu hasahau fimbo yake
 • Kinywa ni jumba la maneno.
 • Kipya kinyemi ingawa kidonda.
 • Kisokula mlimwengu,sera nale.
 • Kitanda usicho kilala hujui kunguni wake.
 • Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua.
 • Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.
 • Kiwi cha yule ni chema cha;hata ulimwengu uwishe.
 • Kobe atakufa asipojikuna nyumaye mwenyewe.
 • Kosa moja haliachi mke.
 • Konzo ya maji haifumbatiki
 • Kozi mwandada, kulala na njaa kupenda.
 • Kufa kikondoo, ndiko kufa kiungwana.
 • Kufa kufaana.
 • Kuchamba kwingi,kuondoka na mavi.
 • Kuku havunji yai lake.
 • Kukopa harusi, kulipa matanga.
 • Kufa kwa mdomo, mate hutawanyika.

Read: 100 Positive Behavior Quotes for Students

 • Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
 • Kuku wa maskini hatagi mayai.
 • Kuku mwenye watoto, halengwi jiwe.
 • Kucha M’ngu si kilemba cheupe.
 • Kufa si suna,ni faradhi.
 • Kujikwa si kuanguka, bali ni kwenda mbele.
 • Kulea mimba si kazi, kazi kulea mwana.
 • Kuagiza kufyekeza.
 • Kunguru mwoga hukimbiza mbawa zake.
 • Kunako matanga kumekufa mtu.
 • Kumpa mwenzio si kutupa, ni akiba ya mbeleni.
 • Kupanda mchongoma ,kushuka ngoma.own.
 • Kupotea njia ndiyo kujua njia.
 • Kutoa ni moyo usambe ni utajiri.
 • Kusikia si kuona.
 • Kuuliza si ujinga.
 • Kutu kuu ni la mgeni.
 • Kwenye miti hakuna wajenzi.
 • Kwenda mbio siyo kufika.
 • Kweli iliyo uchungu si uwongo ulio mtamu.

L

 • La kuvunda (kuvunja)halina ubani.
 • Lake mtu halimtapishi bali humchefusha.
 • La kuvunda halina rubani.
 • Leo ni leo asemayo kesho ni mwongo.
 • Lisemwalo lipo,ikiwa halipo laja.
 • Leo uko, kesho huko.
 • Liandikwalo ndiyo liwalo.
 • Likitoka liote.
 • Lipitalo ,hupishwa .
 • Lifaalo kueleza lieleze, lisilofaa limeze.
 • Lila na fila hazitangamani.
 • Lisilokuwapo moyoni, halipo machoni.
 • Lisilo na mkoma, hujikoma lilo.

Read: Best Quotes about Education

M

  • Macho hayana pazia.
  • Maafuu hapatilizwi.
  • Mafahali wawili hawakai zizi moja.
  • Maisha hayana pato, hutupita kama ndoto.
  • Mahaba haiwi mlango.
  • Maiti haulizwi sanda.
  • Maji ukiyavuliya nguo huna budi kuyaogelea.
  • Maji hufuata mkondo.
  • Maji huteremka bondeni, hayapandi mlima.
  • Maji yakija hupwa.
  • Maji usiyoyafika hujui wingi wake.
  • Maji yakimwagika hayazoleki
  • Maji ya nazi, yataka uvugulio tu.
  • Maji yakija hupwa.
  • Maji yaenda njia yake.
  • Maji ya kifuu ni bahari ya chungu.
  • Maji ya moto, hayachomi nyumba.
  • Majumba makubwa husitiri mambo.
  • Mpanda ngazi hushuka.
  • Majuto ni mjukuu.
  • Mali ya bahili huliwa na wadudu.
  • Mambo ya mbele, giza ya wele
  • Mambo ya nyumba, ni kinga.
  • Manahodha wengi chombo huenda mrama.
  • Maneno mema hutowa nyoka pangoni.
  • Maneno makali hayavunji mfupa.
  • Maneno mengi si haja, maneno mengi si huja.
  • Masikini akipata matako hulia mbwata.
  • Maskini haokoti, akiokota huambiwa kaiba.
  • Maskini na mwanawe, tajiri na mali yake.
  • Masikio hayapiti kichwa.
  • Mapema maivu, mapema maovu.
  • Mapaka wengi, hayamkamati panya.
  • Mapenzi ni kikohozi, hayawezi kufichika.
  • Mapenzi ni majani, popote penye mbolea huotea.
  • Mara changu, mara chako
  • Mavi usioyala,wayawingiani kuku?
  • Mavi ya kale hayanuki.
  • Mbio za sakafuni huishia ukingoni.
  • Mbinu hufuata mwendo.
  • Mbiu ya mgambo ikilia ina jambo.
  • Mbuzi wa maskini, hazai mapacha
  • Mbwa hafi maji, akiona ufuko.
  • Mbinu hufuata mwendo.
  • Mbuge hawezi kujenga nyumba.
  • Mbuzi wa mkata, atakufa utasa.
  • Mchagua jembe si mkulima.
  • Mcheka kilema, hafi bila kumfika.
  • Mchelea mwana kulia hulia yeye.
  • Mchelea bahari si msafiri.
  • Mchagua nazi, hupata koroma.
  • Mchakacho ujao,halulengwi na jiwe.
  • Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo.
  • Mchana semani usiku lalani.
  • Mchele moja mapishi mengi.
  • Mcheka kilema hafi bila kumpata.
  • Mcheza kwao hutuzwa.
  • Mchimba kisima huingia mwenyewe.
  • Mcheza na tope humrukia.
  • Mcheza hawi kiwete, ngoma yataka matao.
  • Mchezea zuri, baya humfika.
  • Mchimba kisima, hakatazwi maji.
  • Mchovya asali hachovi mara moja.
  • Mchonga mwiko hukimbiza mkono wake.
  • Mchuma janga hula na wakwao.
  • Mchumia juani,hula kivulini.
  • Mchuma janga hula na wakwao.
  • Mchunga haziki.
  • Mdharau biu hubiuka yeye.
  • Mema na mabaya ndio ulimwengu.
  • Meno ya mbwa hayaumani.
  • Mficha uchi hazai.
  • Mfa maji hukamata maji.
  • Mfinyazi hulia gaeni.
  • Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
  • Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.
  • Mganga hajigangui.
  • Mfukuzwa kwao hana pakwenda.
  • Mgeni ni kuku mweupe.
  • Mgonjwa haulizwi uji.
  • Mgeni njoo mwenyeji apone.
  • Mgonjwa haulizwi uji.
  • Miye nyumba ya udongo, sihimili vishindo.
  • Milima ya mbali, haina mawe
  • Mjinga akierevuka mwerevu yupo mashakani.
  • Mjumbe hauawi.
  • Mkamatwa na ngozi ndiye mwizi.
  • Mkeka mpya haulaliwi vema.
  • Mkamia maji hayanywi.
  • Mkono moja haulei mwana.
  • Mkono moja hauchinji ngombe.
  • Mkono mtupu haulambwi.
  • Mkono usioweza kuukata, ubusu.
  • Mkosa jembe halimi
  • Mkono wa kuume, haukati wa kushoto.
  • Mkosa kitoweo humangiria.
  • Mke ni nguo ,mgomba kupalilia.
  • Mkosa titi la mama, hata la mbwa hulamwa.
  • Mkulima ni mmoja walaji ni wengi.
  • Mkuki kwa nguruwe mtamu,kwa mwanadamu uchungu.
  • Mla cha mwenziwe na chake huliwa.
  • Mla kuku wa mwenziwe miguu humwelekeya.
  • Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
  • Mla mla leo mla jana kala nini?
  • Mla mbuzi hulipa ngombe.
  • Mla cha uchungu na tamu hakosi.
  • Mla kwa miwili, hana mwisho mwema.
  • Mlenga jiwe kundini hajui limpataye.
  • Mlevi wa mvinyo hulevuka, mlevi wa mali halevuki.
  • Mlimbua nchi ni mwananchi.
  • Mlinzi hulinda ndege, mke mzuri halindwi.
  • Mnyonge hana hasira.
  • Moja shika,si kumi nenda urudi.
  • Mmoja hashui chombo.
  • Mnyamaa kadumbu.
  • Mnywa maji kwa mkono moja,Kiu yake i pale pale.
  • Mnyonyore haunuki, hupendeza maua yake.
  • Mnyonge hupata haki, ni mwenye nguvu kupenda.
  • Moto hauzai moto.
  • Moja shika, kumi hutapata
  • Moja shika si kumi nenda urudi.
  • Moto wa kumvi,hudumu.
  • Mpanda ngazi hushuka.
  • Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.
  • Mpemba akipata gogo hanyii chini.
  • Mpanda ovyo hula ovyo.
  • Mpemba hakimbii mvua ndogo.
  • Mpende akupendaye.
  • Mpofuka ukongweni,hapotewi na njia
 • Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe.
 • Msafiri masikini ajapokuwa sultani.
 • Msema kweli, hana wajoli.
 • Mshoni hachagui nguo.
 • Mshale usiyo na nyoya, hauendi mbali.
 • Msasi haogopi mwiba.
 • Mshale kwenda msituni haukupotea.
 • Msema pweke hakosi.
 • Mshika mawili, moja humponyoka.
 • Msitukane wagema na ulevi ungalipo.
 • Msitukane wakunga na uzazi ungalipo.
 • Msika mavi, hayaachi kumnuka.
 • Msi chake ni mwenda zake.
 • Mstahimilivu hula mbivu.
 • Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba.
 • Mtaka yote hukosa yote.
 • Mtafunwa na nyoka akiona ung’ongo husitika.
 • Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
 • Mtaka unda haneni.
 • Mtegemea nundu haachi kunona.
 • Mtaka yote kwa pupa, hukosa yote.
 • Mtembezi hula miguu yake.
 • Mteuzi hashi tamaa.
 • Mtego bila ya chambo, haunasi.
 • Mtenda mema hasemi, akisema hatendi.
 • Mti hauendi ila kwa nyenzo.
 • Mti huponzwa na tundaze.
 • Mti upigwao mawe ni mti wenye matunda.
 • Mtoto akililia wembe mpe.
 • Mtoto wa nyoka ni nyoka.
 • Mtoto umleyavyo ndivyo akuavyo.
 • Mtondoo haufi maji.
 • Mtoto akibebwa, hutazama kisogo cha mamaye.
 • Mtu hujikuna ajipatiapo.
 • Mtumi wa kunga haambiwi maana.
 • Mtu akimpa maskini kichache, Mungu humruzuku kingi.
 • Mtupa jongoo hutupa na mti wake.
 • Mtu aliyeumwa na nyoka akiona ung’ongo hushtuka.
 • Mtu apandacho (kitu), ndicho avunacho.
 • Mtu pweke, ni uvundo.
 • Mtu asiye na akili, usifuatane naye.
 • Mtu huenda na uchao, haendi na utwao.
 • Mtu hakatai mwito,hukata aitwalo.
 • Mtu halindi bahari, ipitayo kila chombo.
 • Mtu hasafiri nyota ya mwenziwe.
 • Mtu huulizwa amevaani haulizwi amekulani.
 • Mtumi wa kunga haambiwi maana.
 • Mtumikie kafiri upate mradi wako.
 • Mtumai cha ndugu hufa masikini.
 • Mume wa mama ni baba.
 • Mtunza bahari, siye msafiri.
 • Mtumikie kafiri upate mradi wako.
 • Mtulivu hula mbivu.
 • Mtupa jongoo hutupa na mti wake.
 • Mume ni kazi, mke ni nguo.
 • Mungu akikupa kilema, hukupa na mwendo wake.
 • Mume wa mama ni baba.
 • Mungu hapi kwa mvua, wala hanyimi kwa jua.
 • Muhogo mchungu, usiuchezee.
 • Mungu hamfichi mnafiki.
 • Muuliza hujibiwa ili apate fahamu.
 • Mvuvi ajuwa pweza alipo.
 • Mvumbika changa hula mbovu.
 • Mvunja nchi ni mwananchi.
 • Mvungu mkeka.
 • Mvuvi ajuwa pweza alipo.
 • Mwamini Mungu si mtovu.
 • Mwana kila mwaka, ni kubwa baraka.
 • Mwacha asili ni mtumwa.
 • Mwamba na wako hukutuma umwambiye.
 • Mwana maji wa kwale kufa maji mazowea.
 • Mwana mkaidi hafaidi mpaka siku ya Idi.
 • Mwana mkuwa nawe ni mwenzio kama wewe.
 • Mwanadamu atakufa, jina lake litakaa.
 • Mwanamaji, hutaraji kufa maji.
 • Mwanamume ni mbono, hualikia kule.
 • Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura.
 • Mwanga mpe mtoto kulea.
 • Mwana simba ni simba.
 • Mwanzo kokochi mwisho nazi.
 • Mwana wa mtu ni kizushi; akizuka, zuka naye.
 • Mwangaza mbili moja humponyoka.
 • Mwanzo wa ngoma ni lele.
 • Mwanzo wa chanzo ni chane mbili.
 • Mwenda bure si mkaa bure huenda akaokota.
 • Mwenda mbio hujikwa kidole.
 • Mwenye kelele hana neno.
 • Mwenye huba, hana dawa, ila kwa muhibiwa.
 • Mwekaji kisasi haambiwi mwerevu.
 • Mwapiza la nje hupata la ndani.
 • Mwekaji kisasi haambiwi mwerevu.
 • Mwenda tezi na omo marejeo ngamani.
 • Mwenye chake, hakosi cha mwenziwe
 • Mwenye nguvu mpishe.
 • Mwenye pupa hadiriki kula tamu.
 • Mwenye kovu, usidhani kapoa.
 • Mwenye kuchinja hachelei kuchuna.
 • Mwenye shibe hamjui mwenye njaa.
 • Mwenye kutafuta, hakosi kupata.
 • Mwenye shoka hakosi kuni.
 • Mwenye kovu, haliwai na kidonda.
 • Mwenye kovu usidhani kapowa.
 • Mwenye kupenda ni juha.
 • Mwenye kuchinja hachelei kuchuna.
 • Mwenye kisu kikali ndiye alaye nyama.
 • Mwenye kupanda ngazi, na mwenye kushuka ngazi, hawapeani mkono.
 • Mwenye macho, haambiwi tazama.
 • Mwenye kuumwa na nyoka akiona jani hushtuka.
 • Mwenye njaa hana miiko.
 • Mwenye shibe hamjui mwenye njaa.
 • Mwenye tumbo ni tumbole, angafunga mkaja.
 • Mwenzako akinyolewa wewe tia maji
 • Mwili wa mwenzio ni kando ya mwilio.
 • Mwibaji na watwana, mlifi ni mwungwana.
 • Mwiba wa kujitoma, hauambiwi pole.
 • Mwizi, siku zake ni arobaini
 • Mwosha hadhuru maiti.
 • Mwosha husitiri maiti.
 • Mwomba chumvi huombea chunguche.
 • Mzazi haachi ujusi.
 • Mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi.
 • Mzoea punda, hapandi farasi.
 • Mzowea kutwaa, kutoa ni vita.
 • Mzika pembe ndiye mzua pembe.
 • Mzoea udalali, duka haliwezi.
 • Mzungu Wa kula hafundishwi mwana.

N

 • Nahodha wengi, chombo huenda mrama.
 • Nazi mbovu harabu ya nzima.
 • Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu
 • Ncha na ncha, hazichomani
 • Ndugu mwui afadhali kuwa naye.
 • Ndugu chungu, jirani mkungu.
 • Ndege mwigo hana mazowea.
 • Na tuone ndipo twambie, kusikia si kuona.
 • Ndege hulindwa, mke halindwi.
 • Ndimi arobaini, mafundo arobaini.
 • Ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime, wakipatana chukua kikapu ukavune.
 • Ndovu halemewi na pembe zake.
 • Neno ulikataalo, ndilo Mungu apendalo.
 • Ngoja! ngoja? huumiza matumbo.
 • Ngoma ivumayo haidumu.
 • Ngozi ivute ili maji.
 • Ng’ombe haelemewi na nunduye.
 • Ng’ombe avunjikapo guu hurejea zizini.
 • Ngoma ivumayo haikawii kupasuka.
 • Nguruwe aendealo, ndilo atendalo.
 • Nguo za kuazima, hazisitiri matako.
 • Nifae na mvua nikufae na jua.
 • Ni heri mbichi, kama ya kwoka.
 • Ni jambo lipi, lisilo na nduguye, na mwamu wake.
 • Nia njema ni tabibu, nia mbaya huharibu.
 • Nimekula asali udogoni, utamu ungali gegoni.
 • Njia ya mwongo fupi.
 • Njaa ya leo, ni shibe ya kesho.
 • Njema haziozi.
 • Njia ya siku zote haina alama.
 • Nyota haionekani mchana.
 • Nyani haoni kundule, huliona la mwenziwe.
 • Nta si asali nalikuwa nazo si uchunga.
 • Nyoka, mlinzi wa pango lake.
 • Nyumba haikimbii.
 • Nyumba usiyolala ndani huijui ila yake.
 • Nzi kufa juu ya kidonda Si haramu.
 • Nyumba ya udongo haihimili vishindo.
 • Njia mbili zilimshinda mzee fisi, alipasuka msamba.

P

 • Padogo pako Si pakubwa pa mwenzako.
 • Paka akiondoka, panya hutawala.
 • Pabaya pako si pema pa mwenzako.
 • Painamapo ndipo painukapo.
 • Paka wa nyumba haingwa.
 • Paka hakubali kulala chali.
 • Papo kwa papo kamba hukata jiwe.
 • Panapo wengi hapaharibiki neno.
 • Pema usijapo pema; ukipema Si pema tena.
 • Penye kuku wengi hapamwagwi mtama.
 • Penye mafundi, hapakosi wanafunzi.
 • Penye dhiki, hakuna chuki.
 • Penye miti hakuna wajenzi.
 • Penye urembo ndipo penye urimbo.
 • Penye nia ipo njia.
 • Penye wazee haliharibiki neno.
 • Penye wengi pana mengi.
 • Penye wengi pana Mungu.
 • Pesa na zawadi hufanya miadi.
 • Pilipili usozila zakuwashiani?
 • Pwagu hupata pwaguzi.
 • Punda haendi ila kwa kigongo.
 • Punge moja ya mtama, ni bora kuliko almasi.
 • Pofu hasahau mkongoja wake.

R

 • Radhi ni bora kuliko mali

S

 • Samaki mmoja akioza, huoza wote.
 • Sahani iliyofunikwa, kilichomo kimesitirika.
 • Shimo Ia ulimi mkono haufutiki.
 • Shika! Shika! na mwenyewe nyuma.
 • Samaki huanza kuoza kichwani.
 • Shibe ya mtu mwingine hanilazi mnene.
 • Saburi ni ufunguo wa faraja.
 • Shoka lisilo mpini halichanji kuni.
 • Shimo la ulimi mkono haufutiki.
 • Sikio la kufa halisikii dawa.
 • Sikio halilali na njaa.
 • Sikio halipwani kichwa/Sikio halipiti kichwa.
 • Sikio halipwani kichwa.
 • Siku njema huonekana asubuhi.
 • Simba mwenda kimya(pole) ndiye mla nyama.
 • Siku utakayokwenda uchi, ndiyo siku utakayokutana na mkweo.
 • Subira ni ufunguo Wa faraja.
 • Subira yavuta heri, huleta kilicho mbali.
 • Sumu ya neno ni neno.
 • Suluhu haija ila kwa ncha ya upanga.
 • Sitafuga ndwele na waganga tele.
 • Simbiko haisimbuki ila kwa msukosuko.

T

 • Tamaa mbele, mauti nyuma.
 • Teke Ia kuku halimwumizi mwanawe
 • Tamu tulikula sote, na uchungu vumilia.
 • Tonga si tuwi
 • Taratibu ndiyo mwendo.
 • Tabia ni ngozi.
 • Tajiri na maliye,maskini na mwanawe.
 • Taratibu ndiyo mwendo.
 • Titi la mama li tamu.

U

 • Udongo uwahi ungali maji
 • Ukenda kwa wenye chongo, vunja lako jicho.
 • Uchungu wa mwana, aujua mzazi.
 • Ucheshi wa mtoto ni anga Ia nyumba.
 • Ukiona neno, usiposema neno, hutapatikana na neno.
 • Ubishi mwingi, huvuta matata
 • Udugu wa nazi hukutania chunguni
 • Ukiona kwako kunaungua kwa mwenzako kunateketea.
 • Uchwelewapo na jua lala pale.
 • Ujinga wa kuuza si baradhuli wa kununua.
 • Ukiona vinaelea, vimeundwa.
 • Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni.
 • Ukitaka uzuri sharti udhurike.
 • Ukamba hukatika pabovu.
 • Ukiona neno, usiposema neno, hutapatikana na neno.
 • Ulimi hauna mfupa.
 • Ukikosa titi la mama, hata la mbwa huamwa
 • Ukiona zinduna, ambari iko nyuma.
 • Ukila na kipofu sahani moja, usimguse vyanda.
 • Ukienda kwa wenye chongo, vunja lako jicho.
 • Ukipewa shibiri usichukue pima.
 • Ukupigao ndio ukufunzao.
 • Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Fir-Auni.
 • Ukitaja nyoka, shika fimbo mkononi.
 • Ukuukuu wa kamba Si upya wa ukambaa.
 • Ukitaka cha mvunguni, sharti uiname.
 • Ukitaka uzuri sharti udhurike.
 • Ulacho ndicho chako, kilichobaki nicha mchimba lindi.
 • Ulipendalo hupati hupata ujaliwalo.
 • Ulimi unauma kuliko meno.
 • Ulivyoligema utalinywa.
 • Umekuwa bata akili kwa watoto?
 • Umekuwa jeta hubanduki?
 • Umwepuke, mwenda-pweke.
 • Ungalijua alacho nyuki, usingalionja asali.
 • Usiache kunanua kwa kutega.
 • Upikapo samaki, huachi kunuka vumba.
 • Uniponye kwa jua, nitakuponya kwa mvua.
 • Umekuwa nguva, huhimili kishindo?
 • Unamlaumu mwewe, kipanga yuwesha kuku.
 • Ushikwapo shikamana.
 • Usiache mbachao kwa msala upitao.
 • Usigombe na mkwezi, nazi imeliwa na mwezi.
 • Usiyavuke maji usiyoweza kuyaoga.
 • Usitukane wakunga na uzazi ‘ungalipo.
 • Usijifanye kuku mweupe.
 • Usile na kipofu ukamgusa mkono.
 • Usisahau ubaharia kwa sababu ya unahodha.
 • Usisafiriye na nyota ya mwenzio.
 • Usimwamshe aliyelala utalala wewe.
 • Usinivishe kilemba cha ukoka.
 • Usicheze na simba, ukamtia mkono kinywani.
 • Usidharau kiselema chalima kikapita jembe zima.
 • Usipoziba ufa utajenga ukuta.
 • Uta hauui bila upote
 • Uzuri wa mke nguo, wa ng’ombe kulimwa.
 • Uzuri wa mkakasi, ndani kipande cha mti.
 • Uzuri wa godoro wa nje tu, kwa ndani mna pamba
 • Usiwashe taa, nyumbani mwa kipofu.

V

 • Vita havina macho.
 • Vita ya panzi, furaha ya kungu.
 • Vikombe vikikaa pamoja, havina budi kugongana.
 • Vita vya panga, haviamuliwi na fimbo.

W

 • Waraka hauishi maneno.
 • Watafutao, wapata.
 • Wanao usawa gani, hakimu na baradhuli.
 • Wakati wa hari, watu wagombea kisima kimoja.
 • Wapiganapo fahali wawili ziumiazo ni nyasi.
 • Waraka ni nusu ya kuonana.
 • Wema hauozi.
 • Wengi wape.
 • Werevu mwingi, mbele kiza
 • Weka siri moyoni, kunena ni kutolea.
 • Watatuavu, hutatua.
 • Watu wawili hawashibi: mtaka elimu na mtaka ulimwengu.

Y

 • Yu fahali nyati na mali hapati.
 • Yaliyopita, yamepita, yaliyobaki, tuyatupe.
 • Ya kunya, haina wingu.
 • Yapitayo hayabadiliki, na yajayo hayaelimiki.

Z

 • Zito huwa pesi (nyepesi) ukilichukua.
 • Zimwi likujualo halikuli likakwisha.